JNHPP kukamilika Desemba mwaka huu

DODOMA-Serikali imesema imeanza uzalishaji wa umeme kupitia mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, ambapo uzalishaji huo umeanza kwa Megawati 235 kupitia mtambo namba tisa.
Hayo yamesema na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko Bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

“Matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba 2024 kwa mitambo yote nane yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 235 kila moja kuwa inazalisha umeme,”amesema Dkt. Biteko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news