DAR ES SALAAM-Aprili 4,2024 Kamati Tendaji ya Utafiti wa Sekta ya Utalii Tanzania (TTSS) imefanya kikao chake cha kawaida Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Kikao kimejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii kwa ujumla, ikiwa ni pamoja wasilisho la matokeo ya utafiti wa wageni wa kimataifa waliotembelea Tanzania mwaka 2023.