DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendelea na ukaguzi wa Masharti ya Leseni kwa Mabasi ya mjini (Daladala) mkoani Dar es Salaam ambao hufanyika kila siku.
Kufuatia ukaguzi huo, wasafirishaji mbalimbali wamechukuliwa hatua kwa kubainika na makosa mbalimbali kama vile kuzidisha nauli, kuendesha nje ya njia iliyoainishwa kwenye leseni, kujichorea mikanda ikiwemo kukatisha ruti.