LATRA yawataka wamiliki wa mabasi ya Sauli, New Force kujieleza kwa maandishi

DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka wamiliki wa mabasi ya Sauli na New Force yaliyosababisha ajali Machi 28, 2024 kutoa maelezo kwa maandishi kabla ya kuchukuliwa hatua za kiudhibiti.
Siku hiyo majira ya saa 09:42 alfajiri magari matatu yakiwemo ya Sauli na New Force yaligongana katika eneo la Mashamba ya Mpunga wilayani Kibaha mkoani Pwani katika barabara ya Morogoro na kusababisha vifo vya watu wawili, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.

LATRA imesema, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa basi namba T 668 DTF Scania mali ya Mwalabhila Sauli kutaka kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Pia,ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa basi namba T 175 DZU linalomilikiwa na kampuni ya New Force kushindwa kuacha umbali wa gari lililokuwa mbele yake kama inavyopaswa.

Kwa mujibu wa taarifa za Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS), tarehe ya tukio magari namba T 175 DZU na T 668 DTF yalianza safari kutoka Dar es salam kwa pamoja saa 8:44 usiku, ambapo kwa mujibu wa leseni walizopewa, mabasi hayo yalipaswa kuanza safari saa 9:00 na saa 10:30 alfajiri, mtawalia.

Aidha,uchunguzi zaidi kwenye mifumo ya mamlaka unaonesha kuwa madereva wa mabasi hayo wamesajiliwa kwenye mifumo ya mamlaka, lakini hawakutumia vitufe vya utambulisho kwa maana ya i-Button.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news