Menejimenti ya Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF) ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bernard Konga imekutana na Menejimenti ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Yaasin Juma kwa lengo la kujadili na kuweka mkakati wa kushirikiana katika utoaji wa huduma kwa wanachama wa mifuko hiyo. Kikao hicho kimefanyika Aprili 17, 2024 jijini Dar es Salaam.