KAGERA-Zaidi ya shilingi Bilioni 15 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kuchangia ukuaji wa sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini,Wakili Stephen Byabato wakati akiwahutubia wananchi wa manispaa ya Bukoba kwenye Mkutano wa hadhara umefanyika katika viwanja vya Soko kuu la Manispaa hiyo tarehe 14 Aprili, 2024.


Pia,huduma za afya na uchumi kwa wakazi wa Jimbo la Bukoba mjini.
Amesema kuwa, kupitia fedha hizo baadhi ya maeneo ambayo hayakuwa na shule yamepata huduma hiyo kwa kujengewa shule mpya za msingi na sekondari sambamba na kuanzisha huduma za Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Miradi mingine ya mafanikio ni pamoja na uwekaji wa Taa za Barabarani, Marekebisho katika Soko kuu, Usafishaji wa mto Kanoni, Ujenzi wa Hospitali ya wilaya iliyopo Nshambya pamoja na uunganishaji umeme kwa wananchi kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kufuatia kuwepo kwa mafanikio hayo sambamba na uwepo wa mahitaji mengine ya maendeleo, Wakili Byabato ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.

Pia, amekabidhi rasmi kwa wananchi gari la wagonjwa ambalo lilitolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba wamemshukuru Mheshimiwa Rais pamoja na Mbunge kwa jinsi wanavyopambana kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa kiuchumi kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.