DAR ES SALAAM-Aprili 6, mwaka huu Serikali inatarajia kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu jijini Arusha (Samia Suluhu Hassan Stadium).
Hivi karibuni, Serikali ilisaini mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Samia Suluhu Hassan utakaojengwa Kata ya Olmoti jijini Arusha ambapo unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 286.
Dhumuni la kujenga uwanja huo jijini Arusha ni kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya sekta ya utalii kupitia michezo.
Pia,ujenzi wa uwanja huu ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu mwenyeji wa michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027.Mataifa mengine ni Kenya na Uganda.