DAR-Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba kati yetu na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha pamoja na Wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit ambapo Kocha Mkuu huyo ameomba kuvunja mkataba wake kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili nyumbani kwao Algeria.
Mwalimu Abdelhak Benchikha ameueleza uongozi wa Simba kuwa anauguliwa na Mkewe hivyo anahitaji muda kuwa karibu nae na kumuuguza.
Kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hilo Uongozi umeridhia ombi la Mwalimu Abdelhak Benchikha.
Uongozi wa klabu ya Simba unamshukuru Mwalimu Abdelhak Benchikha kwa kipindi chote alichotumikia dani ya timu yetu na tunamtakia kila la heri na tunamuombea Mkewe apate afya njema.
Wakati huo huo, Uongozi wa klabu umemteua Mwalimu Juma Mgunda kukion-goza kikosi akisaidia na Selemani Matola hadi hapo Bodi ya Wakurugenzi itakapotoa uamuzi mwingine.
Mwalimu Juma Mgunda ataanza kazi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaochezwa April 30, Ruangwa Mkoani Lindi katika Uwanja wa Majaliwa.