Msajili wa Hazina ateta na ujumbe kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Perseus

DODOMA-Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, leo Aprili 20, 2024 amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya uchimbaji Madini ya Perseus ya nchini Australia iliyowakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jeff Quartermaine pamoja na Afisa Fedha Mkuu wa kampuni hiyo, Lee Anne de Bruin.
Kampuni ya PERSEUS imenunua hisa za Kampuni ya ORECORP iliyokua inamiliki mgodi wa Nyanzaga uliopo Geita.
Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine, Perseus imekubali kuongeza asilimia 4 ya hisa za Serikali "Free Carried Interests" na kuifanya Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 20 ya mgodi huo kutoka asilimia 16 za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news