Naibu Waziri Pinda azitaka taasisi kushirikiana na tume kuweka mipango ya matumizi ya ardhi

DODOMA-Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda amesema wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Wizara za Kisekta kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Hiyo ikiwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na migogoro ya ardhi inayotokana na jamii za vijijini kuvamia maeneo ya taasisi hizo.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda akikagua Mbanda ya Maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Molena, yanayoendelea wakati wa mkutano wa wadau wa wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi jana jijini Dodoma.

Akitolea mfano ushoroba wa Wanyama ulioko jirani na kiwanda cha Mbolea Minjingu unaoziungunisha Mbuga ya Wanyama Tarangire na Mbuga ya Manyara, Naibu Waziri Pinda amesema,wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi pamoja na Wizara ya Mali Asili na Utalii hazina budi kushirikiana kupima na kuweka mipaka ya ushoroba huo ambao uko hatarini kutoweka kutokana na shughuli za binadamu zinazoendelea jirani na eneo hilo.

Naibu Waziri Pinda amesema hayo mapema jana wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Wadau na Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi alipomwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kufungua Mkutano huo jijini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda akiangalia Kishikwambi kinachotumika kuchakata taarifa za Mfumo wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi alipofika katika Mbanda ya Maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Molena, yanayoendelea wakati wa mkutano wa wadau wa wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi jana jijini Dodoma.

‘’Wizara ya Ardhi iko tayari wakati wote kushirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii katika kubaini maeneo yote ambayo sisi tunaona ni muhimu yakaachwa kwa manufaa ya Taifa,"liongeza Naibu Waziri huyo.

Aidha ameitaka Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kushirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii kuchukua hatua za haraka na mapema ili baadae isije kulazimika kutumia nguvu kuondoa watu katika eneo la ushoroba wa wanayama hao.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Mali Asili na Utalii,  Dunstan Kitandula wakifuatilia jambo wakati wa Maonesho yanayoendelea wakati wa mkutano wa wadau wa wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi jana jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine Waziri Pinda amezitaka mamlaka za upangaji nchini ambazo ni Halmashauri zote nchini kuhakikisha mipango yote iliyoandaliwa kwa kushirikiana na wadau inawasilishwa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi ili ziweze kusajiliwa ili ziweze kupatiwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhandisi Anthony Sanga amewambia wajumbe wa Kikao Kazi hicho kuwa Idadi ya Watu katika Vijiji imekuwa kiongezeka kwa watani wa asilimia 2.4 kwa mwaka akibainisha kuwa vijijini kuna kaya zaidi ya Mil.8.6 sawa na asilimia 60.3 ya Kaya zote nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Eng. Anthony Sanga wa kwanza kushoto, Naibu Waziri Wizara ya Kilimo David Silinde wa pili toka kushoto,Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Mali Asili na Utalii Dunstan Kitandula wakiwa katika Picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa wadau wa wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi jana jijijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Kufuatia hali hiyo Eng.Sanga alisema Ardhi hiyo ikipangwa, kupimwa na kumilikishwa itakuwa inachangia maendeleo ya kiuchumi ikiwemo usalama wa chakula na mtaji muhimu katika kuondoa umasikini hapa Nchini.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi Prof. Wakuru Magigi alibainisha kuwa ifikapo Juni mwaka huu Mipango yote ya Upangaji Vijiji Nchini itakuwa jumla ya Mipango 3,993 ambayo inatekeleza na Mradi wa Uboreshaji Milki Nchini na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi.

Kikao kazi hicho kinajadili miongozo na mada mabalimbali na kutoa mapendekezo pamoja na mikakati itakayosaidia Serikali kuona namna bora ya kuweka utaratibu mzuri ili kuwezesha kuondokana na changamoto zilizopo za upangaji matumizi ya ardhi na migogoro inayowakabili watumiaji anwai wa ardhi pamoja na serilikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news