DODOMA-Aprili 16, 2024 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Caloryne Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na waratibu wa Mradi wa Ushirika wa kimataifa wa kusaidia Maendeleo ya Elimu Global Partnership in Education (GPE) na Ubalozi wa Sweden.
GPE ni mfadhili wa miradi mbalimbali ya elimu nchini ambapo hivi karibuni Serikali ya Tanzania imezindua mradi mwingine mkubwa utakaofadhili na kuboresha kada ya ualimu nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Bi.Lucinda Ramos Akantara (GPE Senior Education Specialist ) na Stella Mayenje (GPE programe Officer from SIDA).