ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zinafanya jitihada kubwa kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na mipango mingine ya maendeleo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Aprili 17,2024 alipofungua rasmi Mkutano wa mafunzo kwa wajumbe na wataalam wa kamati ya SADCOPAC katika kupambana na rushwa , kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa maliasili unaofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar inasimamia masharti na maelekezo ya miongozo ya kamati ya SADCOPAC kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatekeleza kikamilifu makubaliano yaliyoafikiwa baina ya nchi wanachama.