ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuzindua rasmi Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kesho Aprili 14,2024 katika viwanja vya Maonesho ya Biashara, Nyamanzi Mkoa wa Mjini Magharibi.
Sherehe hizo zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Vyama vya Siasa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.