Rais Dkt.Samia ametoa tani 187 za mbegu kwa wakulima Kilombero-Waziri Mkuu

MOROGORO-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa tani 189 za mbegu za mpunga, mahindi na alizeti ili zisambazwe kwa wakulima wa Wilaya ya Kilombero.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wananchi wote walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazonyesha nchini, lakini pia ametoa mbegu hizo ili kuhakikisha wale waliopata athari katika mashamba yao waweze kuendelea na shughuli za kilimo pale hali itakapokaa sawa,” amesema.

Ameyasema hayo leo Jumanne, Aprili 16, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa maeneo ya Mlimba, Taweta, Masagati wilayani Kilombero, mkoani Morogoro ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko. Waziri Mkuu ambaye pia alikagua bonde la mto Kilombero linalojumuisha wilaya tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi, amesema Rais Samia ameelekeza Serikali iendelee kuwahudumia wananchi wote waliopata athari ikiwemo kuimarisha maeneo ya utoaji huduma za afya, kugawa vyakula na kurejesha miundombinu ikiwemo barabara na reli.“Watanzania tuwe watulivu, Serikali yenu ipo kazini. Rais wetu Dkt. Samia ametupa maelekezo ya kuhakikisha tunawahudumia na kurejesha hali, tutaleta vyakula na tayari madaktari takribani 20 wameshasambazwa kwenye mikoa ya Morogoro na Pwani ili waweke kambi za utoaji huduma za afya.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza TARURA, TANROADS na TAZARA zishirikiane kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyopata athari wakati Serikali inasubiri kumalizika kwa mvua ili iweze kufanya ukarabati mkubwa.
Waziri Mkuu anaelekea Ikwiriri, Muhoro na Chumbi wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambako atakagua athari za mafuriko na kuwasalimia wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news