DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua, CPA Anthony Mzee Kasore kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Kabla ya uteuzi huo, CPA Kasore alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Vile vile Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Goodluck Antipas Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati, Shirima ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano Kampuni ya Mafuta ya Puma, Tanzania.