Rais Dkt.Samia awasili Kenya kushiriki Mkutano wa IDA21

NAIROBI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya nchi hizo viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo (IDA21).
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na baadhi ya Watanzania waliofika kumpokea Jijini Nairobi baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.

"Nimewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na kazi ya diplomasia ya kudumisha uhusiano wetu hasa kibiashara na kiuchumi, pia ninahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo (IDA21).Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Ua mara baada ya kupokelewa na Watanzania Waishio Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024.

"Nchi yetu inashirikiana na Benki ya Dunia katika mpango wa IDA kufanikisha miradi mbalimbali inayobadili maisha ya mamilioni ya wananchi katika sekta za elimu na miundombinu,"ameeleza Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news