DODOMA- Serikali imesema Tume ya Uchaguzi (NEC) itabadilishwa jina ifikapo Aprili 12, 2024 na itaanza kutambulika kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.
Taarifa ya Matinyi imesema hatua hiyo inafuatia tangazo la Serikali namba 225 la Machi 29, 2024 la Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024, inayoanza kutumika rasmi Aprili 12, 2024.
“Hivyo, kuanzia Aprili 12, 2024 jina la Tume litabadilika na litakuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi au kwa kiingereza ‘Independent National Electoral Commission.”