Serikali yawataka wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji

DAR ES SALAAM-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ametoa shime kwa Baraza la Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau mbalimbali kutambua mawanda makubwa ya uwekezaji yaliyopo katika nchi yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa (kushoto) wakati wa Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na uwekezaji linalofanyika katika Ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya kimkakati na uwekezaji lilofanyika leo tarehe 27 Aprili, 2024 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.

Waziri Mhagama amesema kuwa, sekta binafsi na wadau mbalimbali waendelee kutoa mapendekezo kwenye fursa mbalimbali zinazojitokeza za kiuchumi ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kiuchumi kufikia malengo yaliyopo.

Ameongeza kusema wananchi wa Tanzania wako tayari, wakiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ameonesha kwa vitendo kwamba yuko tayari hivyo ni vyema kumuunga mkono kwa kufanya kazi ili kujenga uchumi wa Taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya kimkakati na uwekezaji lilofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam 27 Aprili, 2024.

Aidha, jukwaa hilo litasaidia kujenga uelewa wa pamoja juu ya mafanikio yaliyopatikana na katika uwekezaji na ustawi wake wa kiuchumi.

Waziri aliongezea dhana ya kongamano hilo lenye kauli Mbiu ya “Wekeza Tanzania kuongeza thamani ya ziada” linatumika kujenga uchumi imara ambao umeshirikisha Watanzania wengi.

“Na itatutengenezea mazingira mazuri ya biashara ambayo yatachochea wananchi wengi katika uwekezaji na ushiriki wao katika kujenga uchumi,"alisema Waziri Mhagama.

Baraza la Uweshezaji wa Wananchi Kiuchumi limeingia makubaliano na taasisi ya serikali inayosimamia manunuzi ya umma, katika moja ya kipengele katika sheria ya manunuzi ya umma kinachosisitiza kila asilimia 30 ya manunuzi ya umma ya kila mradi yaende kwa vijana, wanawake wazee na watu wenye ulemavu ambayo ni sehemu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) Bi. Beng'i Issa akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama aliposhiriki Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa watanzania katika Miradi ya kimkakati na uwekezaji.

Kwa upande wake Bibi, Beng’i Issa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi wa Kiuchumi (NEEC) amesema,moja ya mambo wanayosimamia ni kuangalia kampuni zinazopata kazi kwenye miradi ya kiuchumi na bidhaa zinazouzwa katika miradi hiyo zinatoka nchini.

Aidha,kwenye ajira Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi linaangalia ajira za moja kwa moja na ajira ambazo sio za moja kwa moja katika uhaulishaji wa teknolojia kwa kusimamia teknolojia nchini na mipango ya kutoa mafunzo ya kuhaulisha inafanyika
Matukio katika picha baadhi ya Washiriki waliohudhuria Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na uwekezaji linalofanyika katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali

Akizungumzia kuhusu kongamano, amesema kongamano hilo la Nne limelenga katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini pamoja na kushirikishana mafanikio na changamoto zilizopo katika ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news