SUA yadhamiria kuleta matokeo chanya Sekta ya Kilimo, Norway yaahidi

MOROGORO-Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Maisha cha Norway umelenga kuifanya Sekta ya Kilimo Tanzania kuwa na ustawi bora kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa Aprili 22, 2024 na Makamu mkuu wa Chuo cha SUA, Prof. Raphael Chibunda wakati wa ziara ya Balozi wa Norway nchini Tanzania,Mheshimiwa Tone Tinnes katika Kampasi ya Edward Moringe mkoani Morogoro.

Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa, ziara hiyo ya Mhe. Balozi Tone ni matokeo ya mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya SUA pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Maisha cha Norway (Norwegian University of Life Sciences).
Amesema, makubaliano hayo yamelenga pia katika kubadilishana uzoefu vyuo vikuu vilivyopo nchini pamoja na vyuo nchini Norway ikiwemo wataalam mbalimbali wa vyuo vikuu, walimu na wanafunzi.

Sambamba na watafiti ikiwa SUA ni chuo kimoja wapo katika kufanikisha makubaliano hayo.
Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Tone Tinnes amesisitiza kuwa, Norway itaendeleza ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, ushirikiano ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 50 mpaka sasa.

Vile vile, Balozi Tone amefurahishwa na kile SUA inakifanya ikiwemo kuelimisha watu hususani wakati huu wa mabadiliko mbalimbali ya tabianchi.

Pia kufundisha watu juu ya kilimo bora na cha kisasa hususani kilimo atamizi na kufanya watu wawekeze kwenye kilimo biashara.
Balozi huyo ameahidi kwa muda wote atakaoendelea kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania ataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kujadili na Makamu Mkuu wa chuo mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya SUA.

Hata hivyo, katika ziara hiyo Balozi Tone ametembelea miradi mbalimbali iliyopo chuoni hapo iliyofadhiliwa na Norway ikiwemo Kituo cha Taifa cha Kuratibu Hewa ya Ukaa ya Kaboni.

Ikiwemo katika kituo cha kujifunzia kilimo atamizi cha kilimo biashara, Maabara ya Sayansi iliyopo Kampasi ya Solmon Mahlangu.
Sambamba na shamba la mafunzo la viumbe maji na kujionea namna ya ufugaji na utunzaji wa samaki aina ya sato na kambale.
Februari, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa ziarani nchini Norway alisaini mikataba mbalimbali ikiwemo mkataba wa kuimarisha sekta ya kilimo, pamoja na hati ya makubaliano ya ushirikiano wa SUA uliosainiwa na Makamu Mkuu wa chuo, Prof. Raphael Chibunda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news