DAR ES SALAAM-Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda Tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya zumma iliyobeba dhima ya “The Best use of Influencers Category for the year 2023”.
Ni kupitia hafla iliyofanyika usiku wa Aprili 5,2024 katika Ukumbi wa St. Peter’s jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zimetolewa na taasisi ya Public Relations Society of Tanzania (PRST).
Afisa Uhifadhi Mkuu na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya TANAPA,Catherine Mbena (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Mheshimiwa Mhandisi Mahundi.
Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi.
Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa unaotolewa na Idara ya Mawasiliano ya TANAPA katika kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya Uhifadhi na Utalii.
Idara ya Mawasiliano- TANAPA imekuwa daraja la kuiunganisha taasisi hiyo na umma, hivyo tuzo hiyo itakuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano kati ya TANAPA, serikali, vyombo vya habari na wadau mbalimbali
TANAPA sasa ni jicho la Nchi kwa kuwa Taasisi inatoa mchango mkubwa kuingiza fedha za kigeni na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kasi kupitia sekta ya utalii nchini.
Pia, imetoa shukrani zao za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza hamasa katika sekta ya utalii na kuitangaza Kimataifa kupitia Filamu ya Royal Tour.
#PRExcellenceAward2023