DAR ES SALAAM-Mtangazaji wa CloudsFM Gadner G. Habash (Captain) amefariki dunia leo Aprili 20,2024 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Wasafi TV, Habash amefariki dunia kutokana na Shinikizo la Damu na atakumbukwa kwa umahiri wake akiwa mtangazaji wa kipindi cha Jahazi.
Gadner aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Kipindi cha Jahazi ambacho alihudumu kwa muda mrefu.
Ikumbukwe licha ya kuhudumu kipindi hicho hadi mwaka 2010 alitangaza kustaafu na baadaye akajiuja na Times Fm.
Hata hivyo, mwaka 2016, Gadner G.Habash aliongezewa dau CloudsFM akarejea tena kuhudumu katika kipindi cha Jahazi hadi hadi umauti unamfika. Mwenyezi Mungu ablaze roho ya marehemu mahali pema. Amen.