TARURA:Paipu karavati zinasambazwa kurudisha mawasiliano barabara za Kilimanjaro

KILIMANJARO-Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro wamenunua na kusambaza paipu karavati kwa ajili ya kurudisha mawasiliano kwenye madaraja yaliyokatika wakati wa mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Nicholas Francis amesema tayari wamepokea fedha za dharura takribani shilingi milioni 477 kwa ajili ya kununua vifaa vya kukabiliana na athari za mvua.

Paipu Kaeavati ni aina ya karavati ambazo zinaweza kuwekwa kwa haraka pale panapotokea barabara imekatika na hivyo huwekwa kwa urahisi na haraka ili kuweza kurudisha mawasiliano kwa wananchi na kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
Mhandisi Francis amesema hadi sasa paipu karavati hizo zimeshasambazwa katika wilaya zote saba ikiwemo Same,Mwanga, Rombo,Manispaa ya Moshi,Moshi Vijijini,Hai pamoja na Siha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news