TBS yatoa leseni za ubora 2,106 kwa wazalishaji

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesema, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wametoa jumla ya leseni za ubora 2,106 kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Aprii 15,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athumani Ngenya katika kikao kazi na wahariri wakiwemo waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

“Ni sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000,"amesema Dkt.Ngenya huku akifafanua kuwa, kati ya leseni hizo, leseni 1,051 zilitolewa bure kwa wajasiriamali wadogowadogo.

“Kuna wajasiriamali wengine wanazo hizo taarifa, kwa hiyo hiyo hao wenye hizo leseni 1,051 sasa hivi bidhaa zao zipo vizuri tumeshathibitisha zinauzwa kwa wepesi bila matatizo na zina nafasi pia ya kutoka nje ya Tanzania kwa maana ya nchi zote za Afrika Mashariki na SADC."

Mbali na hayo amesema, katika kipindi cha miaka mitatu, jumla ya wadau 5,786 kutoka mikoa mbalimbali waliwafikia na kuweza kuwapatia mafunzo.

“Kulingana na bidhaa wanazotengeneza au wanazosindika,TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na kuwawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora na usalama na hatimaye kukidhi ushindani wa soko la ndani, kikanda na Kimataifa.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news