DODOMA-Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Huduma za Tume leo Aprili 29, 2024 imeendesha mafunzo maalum kuhusu utekelezaji wa mfumo wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi (PEPMIS) kwa Maafisa Madini Wakazi wa mikoa jijini Dodoma.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Meneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Fatma Chondo amesema kuwa lengo la mafunzo ni kuongeza ufanisi wa watumishi na kuwezesha Tume ya Madini kufikia malengo ya Serikali hasa kwenye maeneo ya ukusanyaji wa maduhuli, ongezeko la wawekezaji kupitia utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini sambamba na kuongeza ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini.