Tumejipanga kuwahudumia-NHIF

ARUSHA-Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani kufika na kupata huduma za kujisajili na elimu ya manufaa ya bima ya afya katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi- OSHA.
Rai hiyo imetolewa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NHIF, Bi. Catherine Kameka kwenye maonesho hayo yanaendelea katika viwanja vya General Tyre mkoani Arusha.

Mfuko umedhamiria kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kutumia fursa kama hizi za maonesho, tunatoa huduma za kusajili wanachama, kupokea maoni juu ya huduma tunazotoa, kurejesha kadi zilizopotea na kutatua changamoto wanazokuja nazo wanachama wetu, hivyo tunawaomba wafike na tuwahudumie," amesema Bi. Kameka.

Maonesho haya ambayo hufuatiwa na Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani yalianza jana na yanatarajiwa kumalizika Aprili 30, mwaka huu.

Akizungumzia huduma, alisema kuwa Mfuko umejipanga vyema katika kuwahudumia wanachama wake kupitia mtandao mpana wa vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwa na Mfuko.
"Maboresho makubwa yamefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mifumo ya utambuzi wa wanachama wanapokuwa vituoni, huduma zikiwemo za Kibingwa na bobezi lakini pia kusogeza huduma karibu na wananchi," alisema Bi. Kameka.

Kutokana na hayo amewataka kufika katika banda la Mfuko huo ili wapate elimu na hatimaye wachukue hatua ya kujiunga na wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news