Waathirika wa mafuriko Rufiji kujengewa miundombinu ya elimu

PWANI-Serikali kupitia kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itahakikisha miundombinu ya elimu iliyoharibiwa na mafuriko wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani inarudishwa kwa haraka ili wanafunzi waeendelee na masomo.
Kauli imetolewa Aprili 22, 2024 na Waziri wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Adolph Mkenda alipotembelea eneo la mafuriko na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi walioathiriwa na mafuriko hayo.
Katika ziara hiyo, Prof. Mkenda ameagiza wanafunzi wote ambao shule zao zimeathirika na mafuriko, watafutiwe shule mbadala katika maeneo salama katika Wilaya za karibu wakati Serikali inaendelea kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko hayo.

Aidha,katika ziara hiyo, Prof. Mkenda aliambatana na viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) CPA Mwanahamis Chambega na alimuelekeza kuchukua hatua za haraka za kurejesha miundombinu ya elimu kwa waathirika ili watoto hao warejee shuleni.
"Agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona watoto wote wanasoma Tanzania nzima, hivyo ni wajibu wetu kama viongozi, walezi na wazazi kuungana pamoja kukabiliana na changamoto kama hizi za mafuriko kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao," amesema Pro. Mkenda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news