Wakili Mkuu wa Serikali atoa wito kwa watumishi wa ofisi yake

MOROGORO-Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma mahala a kazi ili waweze kufikia malengo yao kwa wakati.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Bonipace Luhende, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakati akifungua Mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Hayo yamesemwa leo Aprili 18,2024 na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende wakati akifungua mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma kwa Wajumbe wa Baraza la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyofanyika mkoani Morogoro.Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (Hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Dkt. Luhende amesema kuwa Kupitia mafunzo hayo wajumbe watajifunza na kuzifahamu vyema Sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma itakayofundishwa na mkufunzi kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora sambamba na mada kuhusu Uendeshwaji wa Baraza la Wafanyakazi Mahala pa Kazi itakayotolewa na mkufunzi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. James Kibamba akichangia mada kuhusu Sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa mada hizi mbili zimelenga kusaidia katika kuwajengea watumishi uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanahusu Utumishi wa Umma hatua itakayosaidia watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi zaidi ikiwa ni amoja na kuondoa migongano inayoweza kujitokeza mahala pa kazi kati ya mtumishi na muajiri wake.
Amefafanua kuwa, Kupitia mada ya kwanza wajumbe hao watapata fursa ya kujifunza Sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kujifunza kuhusu sheria taratibu na kanuni za utumishi wa Umma, katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.Afisa Utumishi Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg. Shukuru Kazembe akitoa mada kuhusu Sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Ameeleza kuwa kupitia mada hizi wajumbe hao watapata nafasi na wasaa mzuri wa kuuliza maswali ambayo yamekuwa yakiwatatiza kwa muda mrefu kuhusu masuala ya kupandishwa vyeo, maslahi ya watumishi na mambo mengine mengi ya kiutumishi ili kuweza kujibu maswali mbalimbali ambayo wamekuwa yakiulizwa kuhusu masuala ya utumishi wa Umma, Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sarah Rwezaura akichangia mada kuhusu Uendeshwaji wa Baraza la Wafanyakazi Mahala pa Kazi wakati wa mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Amewasihi watumishi hao kutumia mafunzo hayo kupata uelewa kuhusu masuala ya kiutumishi ili waweze kufahamu wajibu walionao kwa Waajiri wao na kwa watanzania kwa ujumla kama watumishi wa umma hususani masuala mbalimbali ambayo mwajiri anatakiwa kuwafanyia au kuata kwa kuzingatia kuwa haki na wajibu ni vitu vinavyoenda pamoja.Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka ofisi za mikoa mara baada ya kufungua Mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akiwa katika Picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Kuhusu Uendeshwaji wa Baraza la Wafanyakazi Mahala pa Kazi Dkt. Luhende amesema kuwa mada hii itawasaidia wajumbe wa baraza kupata uelewa kuhusu maana ya baraza la wafanyakazi, sheria, kanuni na miongozo ya uundwaji wa baraza la wafanyakazi, muundo wa baraza la wafanyakazi, kazi za Baraza na umuhimu wa Baraza kwa taasisi za Serikali ikiwemo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Morogoro mara baada ya Mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Kuhusu uwepo wa dhana kuwa Baraza la wafanyakazi ni sehemu ya kupeleka malalamiko ya wafanyakazi Dkt. Luhende amefafanua kuwa dhana hii ni sahihi isipokuwa sio dhana kamili kuhusu uwepo wa Baraza la wafanyakazi kwa kuwa Baraza la wafanyakazi ndio chombo muhimu kwenye taasisi ambacho kikitumika ipasavyo kitasaidia kuleta mafanikio makubwa kwa taasisi husika.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Kiongozi huyo ameleza kuwa ni matarajio yake kwamba uelewa utakaopatikana kupitia mafunzo ya Baraza hili yatasaidia kuwaelimisha watumishi wengine ili kufanya Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuwa na tija katika utekelezaji wa majukumu yao kwa weledi zaidi na kwa wakati.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Mark Mulwambo akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakati akimkaribisha Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (hayupo pichani) ili aweze kufungua Mafunzo kuhusu Haki na Wajibu wa Watumishi katika Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Naye Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Mark Mulwambo Amesema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwa wajumbe ili kuweza kuwajengea uwezo na uelewa mbalimbali kuhusu Utumishi wa Umma na nafasi ya Mabaraza ya Wafanyakazi katika Ofisi za Umma ili yaweze kuwasaidia watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Akiwakumbusha umuhimu wa mafunzo haya Ndg. Mulwambo amesema kuwa mafunzo haya ambayo ni sehemu ya utangulizi wa Baraza la Wafanyakazi ni muendelezo wa kukidhi takwa la kisheria la kuwepo kwa Baraza la Wafanyakazi mahala pa kazi, ambapo OWMS imekuwa ikifanya vikao vyake vya Baraza mara mbili kila Mwaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news