ARUSHA-Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) leo Aprili 30, 2024 wametembelea Makuyuni Wildlife Park iliyopo wilaya ya Monduli katika mkoa wa Arusha kwa lengo la kujifunza Uhifadhi wa wanyamapori na kujionea shughuli za Utalii.
Ziara hii ya mafunzo imefanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa "Tuhifadhi Maliasili" unaoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID).
Mojawapo ya malengo ya Mradi huu ni kuokoa shoroba za wanyamapori zilizoathirika na uvamizi wa binadamu. Na Makuyuni ikiwa ni sehemu ya ushoroba wa Ziwa Manyara/Tarangire ilikuwa ni sehemu sahihi kupatembelea.
Tags
Habari
Makuyuni Wildlife Park
Maliasili na Utalii
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)
TAWA Tanzania