Wananchi Morogoro ondoeni hofu, tupo kazini-TANROADS

MOROGORO-Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro imewataka wananchi wa mkoa huo kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kuchukuwa hatua za dharura kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika katika kipindi hiki cha mvua kubwa.

Akizungumzia athari za mvua hizo Aprili 28, 2024, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba ameeleza kuwa,tayari wakandarasi wapo katika maeneo yote yaliyo athirika na kazi ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo inaendelea.

"Mvua hizi sio Ulanga peke yake ni nchi nzima, lakini kwa Ulanga mwezi Februari liliondoka daraja katika Kijiji cha Mwaya, daraja lile liliondoka kwa sababu ya mafuriko tukapeleka daraja la chuma la dharura, tumejenga daraja kwa wiki mbili kwa sasa hakuna shida panapitika."
Ameainisha maeneo mengine yaliyoathiriwa na mvua hizo ni pamoja na Malinyi, Mlimba, Masagati na Uchendule ambapo pia ameeleza tuelewe kwamba mvua za mwaka huu zimekuwa kubwa kupita kiasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news