Wanne mahakamani kwa kujipatia manufaa ya shilingi 115,000

KATAVI-Aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Ibindi, Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi,Omary Salum Hussein na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani humo.
Washitakiwa kwa pamoja Aprili 9, 2024 wamefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi ECO. 8641/2024 katika Mahakama hiyo mbele ya Mheshimiwa Gasper Luoga.

Shauri hili ni la Jamhuri dhidi ya Omary Salum Hussein na wenzake ambao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi katika Kata ya Ibindi,Musa Buswakala.

Wengine ni Afisa Maendeleo ya Jamii Kata, Obadia Marekani na Kelvin Mayanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Serikali ya Kijiji.

Hati ya Mashtaka ilisomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Kelvin Mwaja, kwamba kwa tarehe tofauti za mwezi Novemba 2022 washtakiwa walitumia madaraka vibaya kwa kuuza Gypsum tisa.

Ni zilizobaki katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ibindi kinyume na Sheria ya Manunuzi na kujipatia manufaa ya shilingi 115,000.

Washtakiwa wamejihusisha na vitendo vya Rushwa kinyume na kifunhu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.

Aidha,washtakiwa wamekana makosa. Mshitakiwa wa kwanza yupo nje kwa dhamana na washtakiwa watatu wamekosa dhamana kwa kuwa hawakuwa na wadhamini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news