DAR ES SALAAM-Watanzania wameshauriwa kutoa maoni kuhusu Muungano ili ushauri huo ufanyiwe kazi na Serikali badala ya kuandika habari mbaya za Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua maonesho ya biashara ya miaka 60 ya Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua maonesho ya biashara ya miaka 60 ya Muungano.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiwa katika uzinduzi wa maonesho ya biashara ya miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Ushauri huo umetolea Aprili 19,2024 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akizindua maonesho ya biashara ya miaka 60 ya Muungano.Mhe. Abdulla amesema, lengo la maadhimisho na maonesho ya miaka 60 ya Muungano ni kujifunza na kuelewa vizuri kazi zinazofanywa na taasisi za muungano pamoja na mafanikio yake.
Ameongeza kwamba, maadhimisho ya mwaka huu yamelenga kuonesha mafanikio ya Serikali zote mbili yaani Tanzania Bara na Zanzibar katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kupitia kauli mbiu inayosema: Miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania: Tumeshikamana, Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa Letu.
Aidha, Makamu huyo wa Rais amewataka watanzania wote kwa pamoja kushirikiana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuulinda na kuuendeleza Muungano wetu kwa ustawi wa Taifa letu.Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) CPA. Mwanahamis Chambega amesema, TEA ni moja kati ya taasisi za muungano ambayo inatekeleza miradi mbalimbali ya Elimu Zanzibar.
Ameongeza kwamba, katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano, TEA inajivunia kufadhili ukarabati wa jengo la hanga, Jengo la utawala na ukarabati wa maabara za sayansi katika Taasisi ya Sayansi ya Karume (KIST) mradi uliotekelezwa kwa takribani Milioni 600.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), CPA. Mwanahamis Chambega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa TEA mara baada ya uzinduzi wa Maonesho ya Biashara ya Miaka 60 ya Muungano kuzinduliwa jijini Dar es Salaam.
Miradi mingine ni ufadhili wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi kwa vijana 600 kutoka Kaya Masikini, ukarabati wa majengo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Pemba, ukarabati na ujenzi wa maabara ya kisasa ya Kompyuta Chuo cha Utawala wa Umma (IPA), ujenzi wa hosteli mbili katika Chuo cha Kiislam Cha Ualimu Pemba zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 kila moja.