Waziri Dkt.Nchemba ateta na uongozi wa IMF-FAD

NA JOSEPH MAHUMI
WASHINGTON DC

WAZIRI wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Ujumbe wa Tanzania (kulia) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD) (kushoto), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Bw. Abdelhak Senhadji, akizungumza jambo wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara hiyo, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (kushoto mstari wa mbele), akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (kulia mstari wa mbele) wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati mstari wa mbele) na Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF walioketi mstari wa nyuma.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news