DODOMA-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya hali ya hewa nchini ikiwemo kufunga miundombinu ya kisasa ya hali hewa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa taarifa ya Serikali bungeni kuhusu changamoto za hali ya hewa nchini na kujibu maswali Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2024.
Pia, kutoa mafunzo kwa watumishi kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa,Kimataifa na kuweka mifumo wezeshi ya usambazaji wa taarifa za hali ya hewa na kuimarisha mifumo ya uhakiki wa ubora wa huduma ikiwemo ununuzi wa rada nchini.
“Nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya hali ya hewa na kuijengea uwezo nchi yetu na kuifanya kuwa kinara Afrika na nje ya Afrika katika masuala ya utabiri wa hali ya hewa;
Hayo ameyasema leo Aprili 25, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Serikali kuhusu changamoto za hali ya hewa nchini.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema, uwekezaji wa miundombinu uliofanyika unajumuisha ununuzi wa rada za hali ya hewa.
Amesema,rada mbili zinakamilishwa kufungwa katika mikoa ya Kigoma na Mbeya huku rada nyingine mbili zikitarajiwa kufungwa Dodoma na Kilimanjaro ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim