DAR-Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema, sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na tija kubwa zaidi kama taasisi za kifedha zitaendelea kuwekeza mitaji katika shughuli za mifugo na uvuvi ili ziweze kuzalisha kwa tija na hivyo kuchangia vyema kwenye pato la taifa.

Amesema sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na tija kubwa katika uchumi wa taifa hivy
ni muhimu taasisi za kifedha ikiwemo CRDB kuendelea kuwekeza mitaji ili kuinua wadau wanaojishughulisha na sekta hizo.
“Nawapongeza CRDB kwa kuaandaa Kongamano hili kubwa la uwekezaji day, ombi langu kwenu, jukwaa hili liwe chachu ya kubadili sekta hizi za uzalishaji kwa kuongeza mitaji ili kuchechemua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,"amesema.