WMA yashiriki Maonesho ya Miaka 60 ya Muungano

DAR ES SALAAM-Wakala wa Vipimo (WMA) imeshiriki katika Wiki ya Maonesho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Maonesho vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Maonesho hayo yalifunguliwa Aprili 19,2024 na Makamu wa Pili Wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ambapo aliwahimiza wananchi kushiriki vyema katika maonesho hayo kwa lengo la kupata elimu na ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi za serikali na binafsi.

Pamoja na mambo mengine, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alizitaka taasisi kuhakikisha zinatoa huduma bora na elimu ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ambazo wanaweza kuwa wanakutana nazo katika taasisi hizo.

Naye, Afisa Vipimo Mwandamizi Jadi Kijumu amesema, Wakala wa Vipimo inatoa elimu katika masuala mbalimbali kuhusiana na matumizi sahihi ya vipimo katika nyanja za biashara,afya,mazingira na zingine za kimaendeleo.

Ili kutanua wigo katika masuala mazima ya vipimo wakala upo kwenye mpango wa kuanza kuhakiki vipimo vyote vitumikavyo katika maeneo ya biashara ikiwemo mita za umeme, vipimo vitumikavyo kwenye upimaji wa muda wa maongezi na intaneti.

"Hii itasaidia kumlinda mlaji kwenye maeneo haya, tuna matumaini kwamba wadau na wananchi kwa ujumla watafaidika vyema na mpango huu,"amesema.
Afisa kutoka Wakala wa Vipimo Bi. Rehema Michael Mgode akitoa elimu kwa Mwananchi aliyetembelea banda la Wakala wa Vipimo katika maonesho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Maonesho haya ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatafikia kilele chake tarehe 25 April,2024 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuhitimishwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo zitafanyika kitaifa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Aidha,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan. Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi na viongozi na wageni kutoka katika mataifa mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news