RIYADH-Meneja wa Klabu ya Al Hilal, Jorge Jesus amesema,msimu wa 2023/24 wa Ligi Kuu ya Saudia Arabia maarufu kama Roshn Saudi League ulikuwa wa kuvutia.
Ni baada ya klabu hiyo kunyakua taji la Ligi ya Roshn Saudi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hazem kupitia mtanange ambao ulipigwa Mei 11, 2024 ndani ya Prince Faisal bin Fahd Stadium.
Ushindi huo uliihakikishia Al Hilal taji la 19 la Ligi ya Saudi Arabia na kuimarisha rekodi yao ya kutoshindwa msimu huu, na kuangazia utendaji bora kwa muda wote.
Ushindi huo, ambao ulihusisha mabao mawili ya Aleksandar Mitrovic, bao la kujifunga la Ahmed Aljuwayd, na mkwaju wa Sergej Milinkovic-Savic, uliiweka Al Hilal mbele ya alama 12 dhidi ya wapinzani wao wa karibu, Al Nassr, zikiwa zimesalia mechi tatu.
Msimu huu, Al Hilal sio tu imesalia bila kushindwa bali pia imeweka rekodi ya dunia kwa kushinda mechi 34 mfululizo katika mashindano yote.
Aidha, Meneja Jesus alibainisha ni jambo la fahari kwa klabu yake kuonesha matokeo chanya nyakati zote.
“Tulichofanikiwa ni kielelezo kwa wengine wote. Tunaongoza kwa mabao ya kufunga, kufungwa machache zaidi, na tuna alama nyingi zaidi. Kando na kushinda ligi, sisi ni washindi wa Super Cup na katika nusu fainali ya Kombe la Mfalme. Tulishindwa tu katika Ligi ya Mabingwa ya Asia."