Azam FC yampa mkataba wa miaka minne Ever Meza Mercado kutoka Colombia

DAR-Azam FC imemtambulisha kiungo mpya, Ever Meza Mercado raia wa Colombia iliyemnunua kutoka klabu ya Leonnes FC (Itagüí Leones) nchini humo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 25,2024 na uongozi wa Azam FC jijini Dar es Salaam.

"Azam FC tunayo furaha kumtambulisha, Ever Meza, kama kiungo wetu mpya tukimnunua kutoka klabu ya Leonnes ya Colombia.

"Meza, raia wa Colombia aliyezaliwa Julai 21, 2000; alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Alianza FC ya huko huko Colombia.
"...amesaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka Azam Complex hadi mwaka 2028.Karibu sana Ever William Meza Mercado.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news