Balozi Kasike ajumuika na mabalozi wengine jijini Maputo kuadhimisha Siku ya Afrika

MAPUTO-Mheshimiwa Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Msumbiji ameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Afrika, akiungana na mabalozi wa nchi nyingine za Afrika waliopo jijini Maputo kuanzia tarehe 22 hadi 25 Mei, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 26,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo, Msumbiji.
Maadhimisho hayo yalifanyika chini ya Kaulimbiu “Elimisha Mwafrika anayefaa katika Karne ya 21" ambapo mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi tarehe 22 Mei, 2024 alikuwa Mhe. Carmelita Rita Namashulua, Waziri wa Elimu na Maendeleo ya Watu wa Jamhuri ya Msumbiji.

Aidha, katika maadhimisho hayo mabalozi walipata nafasi ya kutembelea Chuo cha Mafunzo ya Walimu Chibututuine kilichopo Wilaya ya Manhica na kujionea jitihada zinazofanywa na Serikali ya Msumbiji kuwaandaa walimu wa shule za msingi.
Maadhimisho hayo yalihitimishwa tarehe 25 Mei, 2024 kwa matukio mbalimbali ikiwemo mechi ya mpira wa miguu baina ya Mabalozi wa Afrika na Viongozi wa Serikali ya Msumbiji.

Mhe. Balozi Kasike pia alishiriki kwenye mechi hiyo ambapo mabalozi wa Afrika walishinda kwa mabao 3-2.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news