ARUSHA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa tarehe 03 Mei 2024 amewaongoza Watumishi wa Wizara kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujionea kivutio hicho cha utalii ili kuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza alipowasili Mamlaka ya Ngorongoro, Balozi Mussa amesema Wafanyakazi hao waliokuwa jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, wametumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo ambalo ni la kipekee duniani ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania kupitia njia mbalimbali ikiwemo filamu ya Tanzania: The Royal Tour.
Kadhalika, amesema Wizara kama mdau wa sekta ya utalii nchini imetumia mkutano wa Baraza Kama fursa kwa kuwapa Wafanyakazi nafasi ya kufanya utalii wa ndani, ili kujifunza na kujenga uwezo wa kutangaza kivutio hicho na vingine vingi kikamilifu kutokana na kujionea kwa macho na kupata kwa undani taarifa muhimu kuhusu vivutio hivyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo amewaongoza Wafanyakazi wa Wizara tarehe 03 Mei 2024 kutembelea Mamlaka hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi. Wafanyakazi hao waliokuwa jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, walitumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo la kipekee duniani.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bi. Chiku Kiguhe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Anayesuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa.
Afisa Maliasili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Hifadhi hiyo ambayo aliielezea kama ya kipekee kwa vile ni makazi kwa binadamu na wanyama.
"Si vyema unapomwambia mtu kuhusu kitu fulani wakati wewe mwenyewe hukijui au hujafika, kwani tunaamini kwamba kuona ni kuamini. Hivyo tupo hapa kujifunza na kuwafunza wengine kuhusu utalii wa ndani na tusiwaambie tu wageni kuhusu eneo hili wakati sisi wenyewe hatulijui" amesema Balozi Mussa.
Kadhalika amepongeza jitihada za Mhe. Rais Dkt.Samia za kutangaza utalii hususan kupitia filamu ya The Royal Tour na kusema matunda yake yameonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi wanaotembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Maelezo yakiendelea.
Wafanyakazi wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Sehemu nyingine ya Wafanayakzi wa Wizara.
Wafanayakazi wa Wizara wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
"Filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Mhe. Rais Samia haikutoa matokeo kwa watu wa nje tu bali imetoa matokeo, mvuto na ushawishi hata kwa wananchi wa ndani wakiwemo Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tunaunga mkono na tunatekeleza kile ambacho Mhe. Rais amekianza na kimeleta ushawishi mkubwa kwa watu kutembelea nchini,"amesema Balozi Mussa.
Balozi Mussa ametumia wasaa huo kutoa wito kwa wananchi wa Tanzania na wageni kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea wanyama wakubwa watano maarufu kama "The Big Five" wanaopatikana katika Hifadhi hiyo kama Simba, Tembo, Chui, Nyati na Faru.
Balozi Mussa na Wafanyakazi wa Wizara wakimsikiliza Afisa Maliasili Bw. Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Mamalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara.
Maelezo yakitolewa.
Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai amesema Ngorongoro ni ya kipeee na tofauti na hifadhi nyingine duniani kutokana na binadamu na wanyamapori kuishi pamoja na Mamlaka hiyo ni urithi wa dunia chini ya Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameipongeza Wizara kwa kuitembelea Mamlaka hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wenyeji wake alipowasili katika geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kushoto ni Afisa Maliasili, Bw. Orgoo Mauyai na Wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha kufurahia ziara hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara katika picha.
Msafara wa Magari ya Utalii yaliyobeba wafanyakazi wa Wizara kuelekea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Wizara na Wafanyakazi walipowasili kwenye sehemu maalum ya kuonesha bonde la Ngorongoro.
Picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha za bonde la Ngorongoro linaloonekana kwa mbali.
Picha ya pamoja.
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mussa akiangalia wanyama mbalimbali baada ya kuwasili katika bonde la Ngorongoro. Anayechukua tukio ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Chiku Kiguhe.
Ziara katika bonde la Ngorongoro ikiendelea.
Tembo ambaye ni mmoja wa wanyama mashuhuri watano wanaojulikana kama The Big Five akiwa Ngorongoro.
Viboko nao wanapatikana Ngorongoro.
Pundamilia.
Tembo.
Ziara ikiendelea katika bonde la Ngorongoro.
Pia amewahimiza Wafanyakazi wa Wizara hiyo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kupiga kura ili Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro itetee ushindi wake wa nafasi ya kwanza ya kuwa Kituo Kinachoongoza Kuvutia Watalii Afrika iliyoupata mwaka 2023 kwa kupiga kura kupitia Tovuti ya utalii ya www.worldtravelawards.com. Ili kuwa mshindi wa kipengele hicho kwa mwaka 2024.
Nao Wafanyakazi wa Wizara waliopata fursa ya kushiriki ziara hiyo wameupongeza Uongozi wa Wizara hiyo kwa kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo kwani imewawezesha kufahamu mambo mengi yenye manufaa katika utekelezaji wa majukumu yao na katika maisha yao kwa ujumla.
"Nimefurahi kuwa hapa leo. Nimejionea kwa macho uzuri wa hifadhi hii napongeza viongozi waliofanikisha hili kwani tumejifunza mengi," alisema Bi. Lilian Mushi.