DAR- Mei 23, 2024 Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Michael Battle ametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim (CFR) jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Michael Battle (aliyesimama) akitoa muhadhara wa kidiplomasia kwa baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed.
Akiwa katika kituo hicho, Mheshimiwa Balozi Battle amekutana na kuzungumza na Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kutoa muhadhara wa kidiplomasia kwa baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa kituo pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali aliyoulizwa na wanafunzi.