DAR-Mkurugenzi wa Miliki Bunifu wa Wakala wa Usajili wa Biashara (BRELA), Loy Mhando amesema maadhimisho hayo yalianzishwa WIPO ambapo yatafanyika katika Hoteli ya Johari Rotana huku kauli mbiu ikiwa ni “Miliki Ubunifu na Malengo ya Maendeleo endelevu Kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia Ubunifu”.
“Maadhimisho ya siku ya Miliki Bunifu Duniani huadhimishwa Aprili 26 kila mwaka, lakini kwa hapa kwetu kutokana na tarehe hiyo kuwa na jambo muhimu la kitaifa la kuadhimisha Muungano, sisi tunaadhimisha siku tofauti ambapo mwaka huu tunaadhimishia Mei 9,2024;