BRELA yapata tuzo taasisi bora kidigitali

DAR-Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imepata tuzo katika kipengele cha taasisi bora ya Serikali kidigitali ikiwa ni kutambua mchango bora katika mageuzi ya kidigitali nchini Tanzania.
Tuzo hizo zimeandaliwa chini ya programu iitwayo Funguo Innovation inayosimamiwa na UNDP kwa kushirikiana na Kampuni ya Serengeti Bytes na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) yenye lengo la kutambua michango mbalimbali inayotolewa na Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi nchini katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Tuzo za Kidigitali kwa mwaka 2024 zilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya wiki ya ubunifu ikiangazia mafanikio na changamoto katika ubunifu wa kidigitali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news