Coastal Union FC yaichapa Kagera Sugar mabao 2-1

KAGERA-Coastal Union FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Ni kupitia mtanange uliopigwa Mei 21,2024 katika Dimba la Kaitaba lililopo mjini Bukoba Mkoa wa Kagera.

Shadrack Mulungwe dakika ya 16 na Denis Modzaka dakika ya 69 ndiyo waliwawezesha waajiri wao Coastal Union kung'ara.

Kwa upande wa Kagera Sugar, Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 73 aliwapa bao la kufutia machozi.

Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar kufikisha alama 31 na kubaki nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Vile vile, Coastal Union inafikisha alama 41 huku ikibaki nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news