KATAVI-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Nyanda za Juu Kusini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wametoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Cha Afya cha Mpanda kilichopo mkoani Katavi.
Katika semina hiyo takribani wanafunzi 320 na walimu 12 walipatiwa elimu juu ya madhara yatokanayo na biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na rushwa.
Pia, walielezwa wajibu wao kama wataalamu wa afya katika kuhakikisha ustawi wa jamii na kuepuka uchepushaji wa dawa tiba zenye asili ya dawa za kulevya.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)