PWANI-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Pwani imeshirikiana na Asasi ya Life and Hope Rehabilitation kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa kwa wanafunzi na walimu.
Ni wa Shule ya Sekondari Hassanali Dhamji iliyopo Bagamoyo, wavuvi na wachuuzi wa soko la samaki Bagamoyo.
Katika eneo la soko, elimu ilitolewa kwa kutumia kipaza sauti huku wachuuzi wakiendelea na biashara zao. Pia, waraibu wanaoendelea na tiba ya Methadone walitoa ushuhuda na kuwaasa vijana wasijiingize kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Mwenyekiti wa soko la hilo pamoja na waalimu wa shule ya Hassanali Dhamji wameomba elimu ya dawa za kulevya iwe endelevu katika maeneo yao.
#kataaDawazaKulevyaTimizaMalengoYako
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)