ARUSHA-Ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, imeshiriki Matembezi ya Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani.Maadhimisho hayo yameratibiwa na Asasi ya Kiraia ya Self Awareness for Everyone (SAFE) inayoendesha shughuli zake katika Jiji la Arusha.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hao alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha Dk. Charles Mkombachepa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul C. Makonda.
Matembezi ya Maadhimisho hayo yalianzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhitimishwa katika Viwanja vya Gymkhana jijini Arusha.
Tags
Afya ya Akili
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)