Dkt.Biteko ateta na Balozi wa Marekani nchini

DAR-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Michael Battle kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwamo matumizi ya vyanzo mbalimbali vya nishati ya umeme
Mazungumzo hayo yamefanyika Mei 14, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya umeme ikiwemo upepo, jotoardhi, jua na gesi asilia ikiwa njia mojawapo ya kuchagiza maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Dkt. Biteko amesema kuwa mahitaji ya nishati ya umeme nchini yamekuwa ya kiongezeka kwa kasi kufuatia ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news