Dkt.Yonazi aongoza kikao cha makatibu wakuu cha Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Muungano

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam Aprili 26, 2024 pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kilichohusu kufanya Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam Aprili 26, 2024 pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.

Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake jijini Dodoma na kuhusisha baadhi ya makatibu wakuu Dkt. Yonazi amepongeza na kuwashukuru timu zima ya kamati tendaji kwa namna ilivyotekeleza jukumu hilo na kufanikisha sherehe mbalimbali za Kitaifa nchini.
Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Batholomeo Jungu akiwasilisha taarifa kwa Makatibu Wakuu kuhusu Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024 wakati wa kikao chao Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kilichohusu kufanya Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam Aprili 26, 2024 pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Augustino Tendwa akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa akizungumza jambo wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kilichohusu kufanya Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hoja za kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam Aprili 26, 2024 pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.
Dkt. Yonazi amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kuratibu sherehe hizo kwa mujibu wa taratibu zilizopo na kuhakikisha sherehe zinafanikiwa kwa ufanisi na ubunifu zaidi ili kuendelea kuenzi na kuwa na kumbukumbu za Matukio hayo makubwa kwa Kitaifa.

Aidha,ametumia kikao hicho kukikumbusha Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo na kuzingatia taratibu za utendaji kazi wa Serikalini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news