Dkt.Yonazi atoa maelekezo Wiki ya Tathmini na Ufuatiliaji

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza itumike katika kuongeza Ufanisi na Utendaji wa Shughuli za Serikali ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya kwa Maendeleo ya Taifa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati akifungua kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma tarehe 14 Mei, 2024.
Baadhi ya Washiriki wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza wakifuatilia kikao hicho.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika tarehe 14 Mei, 2024 katika Ukumbi wa NSSF jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajumbe wa kikao hicho kutumia Makongamano hayo kwa lengo la kuonesha fursa zaidi ya kile kinachotarajiwa katika kuwavutia wawekezji nchini.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Rahma Mahfaudh akifafanua jambo wakati wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu akitambulisha wajumbe wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma.

“Yatumieni makongamano haya kwa tija na mshirikishe wadau kwa lengo la kuendeleza ushirikiano na kuchochoea wawekezaji nchini, hivyo Makongamano haya yahusishe sekta za kiuchumi ikiwemo za utalii, uwekezaji pamoja na masuala ya sanaa na utamaduni ili kuchagiza mazingira bora ya biashara na uwekezaji," alisisiza Dkt. Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi (katikati mwenye suti ya blue) akiwa katika picha ya pamoja ya washiriki wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza.

Kongamano hilo la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news