Elimu ya bima yatolewa kwa TAKUKURU Kanda ya Ziwa

MWANZA-Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia Kanda ya Ziwa imetoa elimu ya bima kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza ambapo jumla ya watumishi wapatao 26 wameshiriki mafunzo hayo.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Majukumu ya TIRA, Dhana ya Bima, Bima za Magari, Taratibu za madai, Umuhimu wa kuwa wakala wa bima na bima za Nyumba.

Aidha, mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Kamanda James Ruge na kuhitimishwa na Naibu Kamanda Idrisa Kisaka.

Mafunzo yaliyotolewa ni muhimu katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Utoaji Elimu Kitaifa NIES ambapo TAKUKURU ni miongoni kwa taasisi mojawapo ya kimkakati TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news